BO Togel Bandar Togel Casino Online Bandar Togel Bandar Togel Toto Togel Daftar Togel Bandar Togel Terbesar Slot Gacor BO Togel
KUWATAKIA KHERI WANASUASO KWENYE MITIHANI YA MWISHO WA MUHULA 1,3,5,7,9. - Sokoine University of Agriculture Students Organization (SUASO)

KUWATAKIA KHERI WANASUASO KWENYE MITIHANI YA MWISHO WA MUHULA 1,3,5,7,9.

YAH: KUWATAKIA KHERI WANASUASO KWENYE MITIHANI

 YA MWISHO WA MUHULA 1,3,5,7,9.

 

Ofisi ya Rais wa serikali ya wanafunzi SUASO inapenda kuwapongeza wanafunzi wote kufika mwisho wa muhula wa 1,3,5,7,9 kwani haikuwa kazi rahisi. Sambamba na pongezi hizo Ofisi ya Rais wa serikali ya wanafunzi inaomba wanafunzi kuzingatia mambo yafuatayo;

  1. Kukamilisha usajili wa kozi na kuchapa (print examticket) kabla ya kuingia kwenye mitihani. Hii ni kupunguza usumbufu wowote na kuwa na uhakika wa kumaliza usajili wa kozi.
  2. Kupitia sheria za mitihani nz kuzifuata ili kuepusha usumbufu wakati huu wa mitihani. Kwa kurahisisha bonyeza hapa Examination_regularities_and_Irregularities(1)[1]Ili kupata sheria za mitihani.
  3. Kuzingatia mavazi stahiki ambayo yanaruhusiwa ndani ya chuo na muonekano unaoruhusiwa kama inavyoelezwa kwenye sheria ndogo ndogo za wanafunzi (student bylaws) sehemu ya sita.

Zaidi Uongozi wa serikali ya wanafunzi kupitia Ofisi ya Rais unapenda kuwatakia wanafunzi wote kheri na mafanikio katika mitihani hii ya mwishoni mwa muhula wa 1,3,5,7,9.

 

 

IMETOLEWA NA

George J Temu

Katibu Mkuu Kiongozi SUASO

Related Posts